GOOD WORK DIAMOND, DIAMOND KUSHIRIKISHWA NA WAJE TOKA NIGERIA: PIA WAJE ASEMA DIAMOND NI SUPER ,PIA NI VERY TALENTED. “Waje – I Wish [Official Video]” on YouTube


Kismati cha Diamond Platnumz
kinazidi kuongezeka. Na sasa
muimbaji wa kike anayeaminika
kuwa maarufu na mwenye kipaji zaidi
nchini Nigeria, Waje amemzungumzia
staa huyo wa Tanzania kuwa ni mtu
mnyenyekevu mwenye nidhamu
kubwa ya kazi.

image

“Met this amazing brother yesterday,
humble nd such an inspiration,his
work ethic is super. #
africanlegendsmakingmusic @
diamondplatnumz the talent eh.
Thanks so much for this honour,”
ameandika Waje kwenye Instagram.
Unaweza usiwe unamfahamu vizuri
Aituaje Iruobe maarufu kama Waje
lakini hakuna ubishi kuwa umewahi
kusikia sauti yake. Waje ndiye
msichana anayesikika kwenye hit
single ya P-Square ya mwaka 2008,
Do Me. Na sasa muimbaji huyo
atasikika kwenye wimbo
aliomshirikisha Diamond Platnumz.
DJ Fetty wa Clouds FM
aliyeongozana na muimbaji huyo wa
‘My Number One’ aliandika. “In the
booth right now. Its @
diamondplatnumz featured in @
officialwaje coming ish in Nigeria and
Africa at large,” ameandika Fetty
kwenye kipande cha video
alichokiweka kwenye Instagram.
Katika hatua nyingine, Diamond
amewataka vijana wa Tanzania
kujitikita zaidi kwenye kilimo na
kupotezea ile imani kuwa kilimo ni
ushamba.
“Unajua tusichukulie kama suala la
kilimo kwamba mtu ukilima unakuwa
mshamba,” staa huyo alikiambia
kipindi cha XXL cha Clouds FM jana.
“Unakuwa mtu wa zamani,kwa
sababu unaweza kuwa na swagga
zako na unalima, cha muhimu ni
kuangalia un invest vipi katika kilimo,
katika sector zipi,kuna sector nyingi
sana za kuwekeza katika kilimo.
Kwasababu ukiangalia nguo
tunazovaa,chakula tunachokula,
vyote vinatokana na kilimo, so
ukiweza kujua nitumie fursa gani
kwenye kilimo unaweza kupata pesa
nyingi sana. Ukiangalia hata tajiri wa
kwanza Afrika anatokana na kilimo
‘Dangote’ so unaweza kuajiri watu
kama umebahatika kuwa
nanihii,kwasababu sisi waswahili
wengi sehemu tunazoishi sisi
tunaweza hata kuweka vimatembele
vinini,yani vitu vitu fulani ambavyo
vinaweza vikakusaidia. Na kwa wale
wenye kubahatika wana mashamba
tunaweza tukawaweka watu,
kwamba sisi tunakaa town kuuza
sura,tukawaweka watu ambao
wanatulimia, cha umuhimu ni
kufikiria unalima kitu gani ambacho
kitakuingizia,sio ulime tu mradi
unalima lakini kitu ambacho
kitakuingiza hela kipo. Watu lazima
wale. Tofautisha ukiuza nguo kuna
watu wanaweza wasinunue akavaa
nguo ya jana,lakini mtu hawezi sema
nishakula jana leo sili lazima ale.”
KIPANDE CHA WAJE hicho HAPO

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements