“BONGO REGGAE” ALBUM YA WARRIORS FROM THE EAST KUZINDULIWA DAR.


Kundi kali kabisa la muziki wa
Reggae hapa Tanzania, Warriors
From The East wamewataka
mashabiki wao kukaa tayari kwa
uzinduzi mkubwa wa albam yao
mpya ambayo inakwenda kwa jina
Bongo Reggae, utakaofanyika hivi
karibuni kwa onyesho kubwa jijini
Dar.

image

Warriors From The East
eNewz imeongea na wasanii wa
kundi hili, Black Jesus na Ras Magere
kuhusiana na albam hii mpya
ambayo tayari imekwishakamilika,
ambapo wamesema ni kazi tofauti
na yenye vionjo vya kitanzania, ikiwa
na ladha mpya kabisa kwa wapenzi
wa muziki wa Reggae.
Wasanii hawa pia wamewaomba
mashabiki zao kuwapigia kura
kuwawezesha kushinda tuzo za
muziki kutoka Kilimanjaro Music
Awards 2014, ambapo wameweza
kuingia katika kinyang’anyiro kwa
mara nyingine tena mwaka huu.
SOURCE: E’NEWS

Posted from WordPress for Android,by hailedavy