FAIDA TANO (5) ZA KUSOMA KWA NJIA YA MTANDAO (ONLINE )


Kukua na Kuongezeka kwa
teknolojia , kuongezeka kwa idadi ya
wanafunzi duniani hivyo basi hata
elimu namna ya kuipata imebadilika.
Unaweza kusoma kwa njia ya
mtandao na haulazimiki kwenda
chuoni kila siku au mara kwa mara
ilimradi uwe na komputa yenye
intaneti. Ingawa watu wamekuwa
wakiichukulia kwa ugumu kidogo
ukilinganisha na kuhudhuria darasani
kila siku, wanafunzi wanaosoma kwa
njia ya mtandao wanaonyesha
kuridhika zaidi na elimu zao na
hufanya vizuri zaidi kwenye matokeo
yao.
Kusoma kwa njia ya mtandao kuna
faida nyingi, zifuatazo ni baadhi tu:

image

1. Urahisi wa kusoma
Inawezekana watu wengi wanapenda
kusoma kwa njia ya mtandao hasa
hasa nchi zilizoendelea ni kwasababu
ya urahisi wake wa kusoma.
Mwanafunzi anapata faida asomee
wapi saa ngapi na lini. Haimaanishi
masomo ni mepesi , hii inamaanisha
hautatakiwa kwenda darasani kwa
muda maalumu kitu ambacho
kinasaidia watu wenye familia au
wanaofanya kazi ambazo
zinawabana sana.
2. Uwezo wa kupata masomo kwenye
mtandao
Kitu unachohitaji ni komputa na
intaneti tu, hivyo unapata na kuweza
kusoma kitu alichofundisha mwalimu
kwa njia ya video, sauti na hata
nakala za maandishi ya kawaida.
Mfumo huu unakufanya kurudia kitu
kama hujaelewa na hupotezi kitu,
kuliko madarasa ya kawaida
mwalimu akishafundisha ukisahau
na kama hukuandika inakuwia
vigumu kukumbuka alichokisema au
alichoelezea.
3. Mawasiliano na mwalimu wako
Mwalimu siku zote anapatikana kwa
njia ya barua pepe au simu,
hautasubiri mpaka umfuate ofisini au
masaa ya kazi. Vilevile unapata
matokeo yako haraka kwa kuwa kila
kitu unakifanya kwa njia ya mtandao.
Hivyo inakuongezea kuwajibika na
unakuwa unajua mwenendo wa
masomo yako mara baada ya
kumaliza kufanya mazoezi ya somo
au majaribio ya somo.
4. Gharama zake ni ndogo
Gharama utakayo lipa ni ada tu ya
mwaka, ambayo inakuwa rahisi
kuliko elimu ya kawaida ya kuingia
darasani. Vilevile hutahitajika kulipia
vitu kama vitabu, hosteli, gharama za
kujiandikisha n.k
5. Huna ugomvi na mwalimu au
mkufunzi wako
Zile tabia za mwalimu kumfuatilia
mwanafunzi, kwa njia ya mtandao ni
ndogo au hamna kabisa. Hivyo
msongo wa mawazo wa kupunjana
maksi kwa sababu ya mambo binafsi
na mkufunzi hayapo.
#SOURCE: BONGO5

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements