Victoria Kimani kuja na reality Show iitwayo “THE RISE OF THE QUEEN” on YouTube


Mwimbaji wa Chocolate City Music
Mkenya Victoria Kimani kwa
kushirikiana na Reel TV anatarajia
kuja na reality TV show yake iitwayo
‘The Rise of The Queen’ ambayo
itakuwa ni series yenye mkusanyiko
wa matukio mbalimbali ya behind
the scenes katika shughuli zake za
muziki.
Victori ambaye alikuwa Tanzania
mwezi uliopita kwaajili ya
kujitangaza zaidi na kuutangaza
muziki wake, amekuwa akifuatana na
crew yake ya production ambao
wamekuwa wakirekodi matukio
mbalimbali wakati wa interviews
zake, studio session wakati akirekodi,
pamoja na shows zake kwa miezi
kadhaa iliyopita, japokuwa alipokuja
Tanzania hakuongozana nayo hivyo
tutayakosa matukio ya Tanzania.
Usihangaike sana kubadilisha station
katika king’amuzi chako kuitafuta
reality show hiyo, sababu itakuwa
ikipatikana kupitia channel yake ya
Youtube kila wiki, na inatarajiwa
kuanza kuonekana wiki ijayo April 8.
Episode mpya zitakuwa zinawekwa
Youtube kila Jumanne.

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements