VIDEO YA WIMBO WA NAKUPENDA YA MAFIKIZOLO ITAFANYIKIA KATIKA ARDHI YA TANZANIA NA DIRECTOR ATAKAEONGOZA ATAKUWA MTANZANIA.


Kundi la muziki la Mafikizolo kutoka
Afrika Kusini ambalo lipo nchini
kwajili ya show moja itakayofanyika
leo Mlimani City, lina mpango wa
kufanya video ya wimbo wao mpya
‘Nakupenda’ hapa Tanzania kabla ya
kuondoka.

image

Theo Kgosinkwe and Nhlanhla Nciza.
“Tungependa kufanya video ya
Nakupenda hapa Dar kwani jina la
wimbo ni la kiswahili na itapendeza
hivyo, bado hatujapata director wa
kufanya video hii ila ndio mpango
wetu”waliiambia Sammisago.com
Pia Mafikizolo wamesema
wamefanya mabadiliko makubwa
katika muziki wao ili kukidhi haja za
bara zima la Afrika.
“mabadiliko ya muziki wetu
yalifanyika ili kuteka soko la bara lote
la Africa na zaidi ikiwezekana ndio
maana Khona na Happiness zina
miondoka tofauti”. Alisema Nhlanhla
Nciza
Katika hatua nyingine Mafikizolo
wamethibitisha kuwa wanampango
wa kufanya kazi na msanii mkubwa
kutoka Tanzania atakaye tajwa hivi
karibuni na collabo hii ndio chanzo
cha kuboresha mahusiano mazuri na
wasanii wa Tanzania.
Source:Sammisago.com

Posted from WordPress for Android,by hailedavy