WATU WATATU (3)WAHUKUMIWA KIFO INDIA KWA KOSA LA KUBAKA


image

Maandamano ya kupinga ubakaji
India
Wanaume watatu wamehukumiwa
kifo Mjini Mumbai, India baada ya
kupatikana na hatia katika visa
tofauti vya ubakaji walioufanya kwa
pamoja.
Moja ya visa hivyo kilitokea dhidi ya
mwandishi mpiga picha aliyekuwa
kazini alipobakwa.
Uamuzi huo umefanywa chini ya
sheria mpya iliyopitishwa ya
kuwaadhibibu wanaoendeleza uhalifu
huo wa ubakaji.
Sheria hiyo ilipitishwa baada ya kile
kisa Delhi kilichoughadhabisha
umma cha msichana aliyebakwa na
ngege basini na kujeruhiwa vibaya
sana.
Wanaume hao walikuwa
wameshitakiwa kwa kesi ya kumbaka
msichana huyo mwandishi aliyekuwa
ameenda kupiga picha kiwanda cha
nguo kilichotelekezwa, lakini pia
mwanamke mwengine akajitokeza
na kutoa ushahidi wa jinsi wanaume
hao walivyombaka maeneo hayo
hayo mwezi mmoja kabla.
Wahukumiwa hao wanaweza kukata
rufaa kwa mahakama ya juu zaidi.
Kuongezaka kwa visa vya ubakaji
vimepelekea maaandamano ya mara
kwa mara nchini humo na sasa
mahakama zinaharakisha kusikilizwa
kwa kesi hizo.
Pia limekuwa swala la mijadala
mikali katika kampeni za uchaguzi
unatajariwa hivi karibuni nchini
humo.

image

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements