BIRDMAN AMZAWADIA JUSTIN BIEBER GARI AINA YA BUGGATI


image

Birdman na Justin Bieber
Muanzilishi na mmiliki wa studio ya
Cash Money, mjasiriamali na rapa
Brayan Williams(45) ‘BirdMan’
amemzawadia mwanamuziki wa
R&B, Justin Bieber gari ya kifahari
aina ya ‘Bugatti Veyron’ yenye
thamani ya dola za kimarekani
milioni 2 alilokuwa akitumia hapo
awali.
“Uncle Stunna luv. My first Bugatti ♛
#generosity,” aliandika Justin Bieber
kwenye ukurasa wake wa Instagram
sambamba na kuweka picha ya
mkoko huo wa bei chafu.

image

Katika picha ni gari aina ya Bugatti
aliloposti Justin Bieber Instagram
baada ya kupewa kama zawadi na
Birdman.
Kwa wale wafuatiliaji ni kwamba,
gari alilopewa Justin Bieber ndio
alilolitumia BirdMan kwenye video ya
wimbo wake wa ‘Fire Flame’ iliyotoka mwaka2010•