MSAKO DHIDI YA WAGENI WAENDELEA KENYA


image

Msako Kenya waendelea
Maafisa wa Polisi nchini Kenya
wanasema wamekamata zaidi ya
watu elfu tatu katika msako dhidi ya
wageni nchini humo .
Msako huo ulianza Ijumaa, baada ya
mashambulizi ya gurunade wiki
iliyopita katika eneo la Eastleigh
linalokaliwa zaidi na wasomali katika
mji mkuu Nairobi.
Wengi wa waliokamatwa ni
wasomali .
Inspekta mkuu wa polisi , David
Kimaiyo, amesema kuwa watu 450
bado korokoroni asili mia kubwa yao
ikiwa katika uwanja wa michezo wa
Kasarani huku waliosalia
wakiruhusiwa kwenda zao baada ya
kuchunguzwa na maafisa
wa usalama na wale wa uhamiaji
kubaini uhalali wao .
Umoja wa Mataifa, makundi ya
kutetea haki za binadamu na jamaa
wa watu hao wanasema hawajapewa
ruhusa ya kuwaona wapendwa wao.
Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya
Joseph Ole Lenku, anasema wale
ambao hawana vibali vya kuishi
nchini watachukulia hatua zaidi.
Sitini na tisa wamepelekwa
mahakamani kwa madai ya kuwepo
nchini Kenya bila idhini au kumiliki
stakabadhi gushi.

image

Msako Kenya waendelea
Mwandishi wetu Robert Kiptoo
ambaye amezuru mtaa huo wa
Eastleigh ametueleza kuwa msako
wa polisi dhidi ya wahamiaji haramu
na washukiwa wa ugaidi bado
unaendelea .
Msemaji wa polisi nchini Kenya
Masoud Mwinyi amekanusha madai
kuwa polisi wanalenga jamii moja
ama watu wa dini moja.
Mashirika ya kijamii na yale ya
kutetea haki za kibinadamu
yanalalamika kuwa yamenyimwa
fursa ya kuwatembelewa washukiwa
hao waliokamatwa.
Miongoni mwa waliokamatwa ni raia
wa Kenya, Uganda, Sudan, Sudan
Kusini ,hata hivyo idadi kubwa
inatoka Somalia.
Aidha ripoti zinasema kuwa wageni
wengi wamekimbilia miji mingine
nchini Kenya kukwepa msako huo wa
polisi lakini.
Serikali imetoa onyo kwa Wakenya
kutowasaidi watu ambao
wanawashuku kuwa wageni.
Serikali ya Kenya imeonya kuwa
haitawavulimia wakimbizi mijini
ikisema kuwepo kwao mijini
kunahujumu usalama wa taifa.