RUSSIA YATOA ONYO KWA UKRAINE


image

Wanaharakati wanaopendelea Urusi
kutoka Ukraine
Urusi imeionya Ukraine kuancha
maandalizi yoyote ya kijeshi kusini
na mashariki mwa nchi hiyo, ikisema
kwa kufanya hivyo kutaanzisha vita
vya wenyewe kwa wenyewe.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje
ya Urusi imesema Ukraine ilikuwa
ikipanga kupeleka majeshi yake
katika maeneo hayo, ikituhumu
kwamba makandarasi binafsi wa
kijeshi wa Marekani ni miongoni
mwa watu waliokuwa katika mpango
huo.
Onyo la Urusi limekuja baada ya
serikali ya Ukraine kusema kwamba
wanaendesha operesheni dhidi ya
ugaidi wakati wa usiku katika jengo
la utawala katika mji wa mashariki
ya Ukraine wa Kharkiv na
kuwakamata watu sabini
wanaoiunga mkono Urusi ambao
waliliteka jengo hilo. Jumatatu,
wanaharakati wanaopendelea
kujiunga na Urusi kutoka majimbo ya
Kharkiv na Donetsk wametangaza
kujitenga na Ukraine. (Urusi
imekanusha kuchochea kukosekana
kwa utulivu na mawazo ya kujitenga
kwa maeneo nchini Ukraine.)