WATU WANNE (4).WATUPWA JELA KWA KUJIHUSISHA NA MAPENZI YA JINSIA MOJA NCHINI MISRI


image

Wanne wahukumiwa kifungo jela kwa
kosa la kujihusisha na mapenzi ya
jinsia moja nchini Misri
Mahakama moja nchini Misri
imewahukumu watu wanne kifungo
cha hadi miaka minane jela kwa kosa
la vitendo vya kufanya mapenzi ya
jinsia moja.
Watu hao wanashutumiwa
kuhudhuria au kupanga tafrija za
vitendo vya ngono, na kuvaa mavazi
ya kike na kujipodoa.
Sheria ya Misri haitamki kupiga
marufu vitendo vya mapenzi ya jinsia
moja, lakini waendesha mashitaka
wametumia sheria ya Misri
inayokataza mambo fulani kufanyika
hadharani kuwahukumu wapenzi wa
jinsia moja.
Hukumu hiyo imeshutumiwa na
wanaharakati wa haki za binadamu.
Mmoja wa watu hao amehukumiwa
na mahakama mjini Cairo, kifungo
cha miaka mitatu jela na kazi ngumu.
Kikundi cha kutetea haki za
binadamu chenye makao yake nchini
Marekani, Human Rights First ,
kimesema hukumu hizo zinasikitisha
na kukatisha tamaa.
“Misri ni taifa linalobadilika katika
eneo la nchi za Kiarabu;
kinachotokea Misri kinaweka hali ya
kuenea katika ulimwengu wote wa
nchi za Kiarabu,” kimesema kikundi
hicho katika taarifa yake.
Kikundi hicho kimesema tangu
kung’olewa madarakani Rais
Mohammed Morsi mwezi Julai 2013
kumekuwa na ongezeko la watu
kukamatwa kwa misingi ya jinsia
zao.
Hukumu ya sasa inakumbushia kesi
ya mwaka 2001 ya watu 52
kushutumiwa kwa vitendo vya
mapenzi ya jinsia moja na makosa
mengine chini ya sheria ya Misri.
Watu ishirini na watatu
walihukumiwa kifungo cha kufikia
miaka mitano jela pamoja na kazi
ngumu, hukumu ambayo
ilishutumiwa kimataifa.
Kikundi kimoja cha kutetea haki za
binadamu nchini Misri kimesema
adhabu kali zilizotolewa kwa watu
hao Jumatatu ni sehemu ya msako
unaoendelea dhidi ya uhuru binafsi.
Credit: BBC NEWS