WATU ZAIDI YA ELFU NNE (4,000) WAKAMATWA NCHINI KENYA


image

Watu waliokamatwa katika msako
mjini Nairobi wakiingizwa uwanja
wa mpira wa Kasarani
Serikali ya Kenya imesema kwa sasa
inawashikilia zaidi ya watu elfu nne
kufuatia operesheni usalama nchini
humo.
Msako huo wa kamatakamata
ulianza baada ya mashambulio ya
magruneti wiki iliyopita katika eneo
la Eastleigh jijini Nairobi, ambalo
wakaazi wake wengi ni wa jamii ya
Kisomali.
Wengi wa watuhumiwa ni Wasomali.
Wengi wao wanashikiliwa kwa siku
tatu katika uwanja wa mpira wa
Kasarani jijini Nairobi. Umoja wa
Mataifa, makundi ya kutetea haki na
ndugu wa watu waliokamatwa
wamesema wamenyimwa nafasi ya
kukutana na watuhumiwa hao.
Waziri wa mambo ya Ndani wa
Kenya, Joseph Ole Lenku, amesema
wale ambao hawana vitambulisho
kuhusu ukaazi au uraia wao wa
Kenya, watafikishwa mahakamani na
huenda wakarejeshwa Somalia.
Credit: BBC TV’

Advertisements