KENYA YAWAREJESHA MAKWAO WASOMALI ZAIDI YA 80


image

Kenya yawaregesha Wasomali
Nyumbani
Serikali ya Kenya imewarudisha
nyumbani Wasomali 82 waliokuwa
miongoni mwa wageni 3000
walioshikwa katika msako mkubwa
unaoendelea mjini Nairobi
kukabiliana na tishio la ugaidi.
Mwandishi wa BBC mjini Nairobi,
Paul Nabiswa, ambaye yuko katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Jomo Kenyatta ameshuhudia zaidi ya
Wasomali 82 wakiingizwa katika
ndege moja ambayo
imekodishwa maalum kwa shughuli
hiyo.
Balozi wa Somalia nchini Kenya ,
Mohammed Nur amesema kuwa
ndege hiyo imekodishwa na serikali
ya Somalia baada ya watu hao
kuamua kwa hiari yao wenyewe
kurejea nyumbani baada ya
kukamatwa katika msako
unaoendelea mjini Nairobi wakiwa
hawana vibali rasmi ya kuishi nchini
Kenya.
Balozi huyo anasisitiza kuwa
wasomali wengi wakimbizi
walionaswa wakiwa na stakabadhi
rasmi za Shirika la umoja wa mataifa
linaloshughulikia wakimbizi UNHCR
wataregeshwa katika kambi za
wakimbizi baada ya uchunguzi wa
serikali ya Kenya.
Msako huu unaoendelea sasa mjini
Nairobi ulianza ijumaa iliyopita
baada ya kutokea milipuko ya grenadi
mtaani Eastleigh .
Watu sita waliuawa katika matukio
hayo ya mwisho yaliyoibua hasira
miongoni mwa wakenya na
kuchochea serikali kuanzisha msako
huu.
Kufikia jana Polisi ya Kenya
ilidhibitisha kuwa imewanasa
wahamiaji 3,000 na kuwaachilia
huku ikiwa imesalia na wahamiaji
447 .

Advertisements