MATUMAINI YA KUPATIKANA KWA MH 370 YA MALAYSIA BADO YANAENDELEA.


image

Operesheni ya kuitafuta MH 370
inaendelea.
Kiongozi wa operesheni ya kuitafuta
ndege ya Malaysia ya MH370
iliyotoweka mwezi mmoja uliopita,
Angus Houston wa Australia,
amesema kuwa ametambua
mawimbi ya sauti inayoaminika
kutoka kwa kinasa sauti cha ndege
hiyo maarufu kama ‘black box’ ya
ndege hiyo.
Houston alisema kuwa kifaa
maalumu kinachokokotwa na meli
moja ya kijeshi ya Australia, Ocean
Shield, kilipata mawimbi kamili kwa
muda wa kati ya dakika tano u nusu
na saba.
Mawimbi sawa na hayo
yaliopatikana mwishoni mwa wiki na
hii ina maana kuwa wataweza
kulenga eneo ambalo inaaminika
zaidi kuwa ndege hiyo ilianguka na
kwa hivyo kuimarisha utafutaji wake.

Advertisements