UKRAINE YAPEWA SAA 48 KUAMUA MUSTAKABAL WAO


image

Majengo yaliyotekwa mashariki ya
Ukraine
Waukraine wanaoishi mashariki mwa
taifa hilo wanatakriban saa 48
kuamua mustakabal wao la sivyo
wakabiliane na vyombo vya usalama
vya dola.
Waziri wa masuala ya ndani nchin
Ukrain Arsen Avakov amewaambia
waandishi wa habari mjini Kiev kuwa
hali iliyo mashariki mwa nchi
itatatuliwa kstika masaa 48 yajayo
aidha kwa mazungumzo au kwa
kutumia nguvu.
Wanaharakati wanaoiunga mkono
Urusi bado wameyateka majengo ya
serikali kwenye miji miwili iliyo
mashariki mwa Ukrain
Duru zinaarifa kuwa baadhi ya
waandamani ambao walikuwa
wameteka majengo ya serikali katika
mji wa Luhansk wameondoka .
Mapema juma hili utawala nchini
Ukrain uliendesha kile ulichokiita
kampeni dhidi ya ugaidi ukilenga
makundi yaliyotenga.
Ukrain inaishutumu Urusi kwa
kuchochea ghasia.
Maafisa wa ngazi za juu kutoka
Urusi, Marekani , Ukrain na Jumuiya
ya Ulaya wamekubalina kufanya
mazunguzmo juma lijalo.

image

Majengo yaliyotekwa Donetsk
Mazungumzo hayo yanalenga kuleta
uwiano baada ya Urusi kuteka eneo
la Crimea mwezi February .
Majeshi ya Urusi yangali karibu na
mpaka wa Ukraine .
Taharuki imetanda mijini Luhansk,
Donetsk na Kharkiv tangu watu
wanaounga mkono hatua ya Urusi
kuchukua Crimea kudai wanataka
Urusi itawale miji hiyo iliyoko
mashariki mwa Ukraine.
Serikali ya Kiev tayari imewataja
kuwa magaidi na kuwa inapanga
operesheni dhidi ya magaidi hao
katika kipindi cha siku mbili zijazo.
Bwana Avakov amesema kuwa afua
ni mbili mazungumzo ya amani ama
vita.
Kiongozi wa waandamani mjini
Luhansk amemuaomba rais wa Urusi
Vladimir Putin kuwasaidia
wasidhulumiwe na Kiev.
Wakati huohuo serikali ya Kiev
imetangaza kuwa imewaachia watu
56 waliokuwa wamekamatwa kwa
kuvamia majengo ya Umma.
Huko Kharkiv viongozi wa
maandamano wamelaumu serikali ya
Kiev kwa matatizo mengi
yanayowakumba na wakaitisha kura
ya maoni ya kuamua iwapo
wangependa kusalia Ukraine ama
kujiunga na Urusi.
Vyombo vya habari vimeripoti kuwa
kiev imetwaa majengo yaliyokuwa
yametekwa na waandamanji
ingawaji hali ingali tata katika mji
ulioko karibu wa Donetsk.

Advertisements