GERRIE NEL AFANYA MAHOJIANO NA OSCAR PISTORIUS


image

Mwendesha mashtaka Gerrie Nel
akimhoji Pistorius
Mwendesha mashata wa serikali
nchini Afrika Kusini ameanza
kumhoji mwanariadha mlemavu
Oscar Pistorius ambapo amemtaka
akiri kumuua mpenziwe Reeva
Steenkamp mwaka uliyopita.
Akimhoji Pistorius wakati wa siku
yake ya tatu ya kutoa ushahidi Gerrie
Nel alimtaka Pistorius kukubali
kumuua mpenziwe nyumbani kwake
februari tarehe 14.
Pistorius hata hivyo alijibu kwa
kusema kuwa alikuwa amefanya
makosa na hakutarajia kumuua
Reeva Steenkamp.
Mwanaridha huyo amesema kuwa
alifyatua risasi zilizomuua mpenziwe
akidhani kuwa ni jambazi aliyekuwa
amevamia nyumba yake.

image

Pistorius akiwasili mahakamani
Pretoria
Awali Oscar Pistorius alielezea hali
ilivyokuwa punde baada ya kumpiga
risasi mpenziwe wa kike Reeva
Steenkamp nyumbani kwake.
Wakati wa ushahidi wake wenye
majonzi mengi Mwanariadha huyo
alisema kuwa Steenkamp alifariki
mikononi mwake hata kabla ya gari
la wagonjwa mahututi halijafika.
Alisema alijaribu kumsaidia ili
apumue huku akizuia damu
kububujika zaidi kutoka kiunoni
mwake.
Viongozi wa mashtaka wana imani
kuwa alimuuwa kimakusudi ndani ya
choo chake kwenye bafu baada ya
kuzozana.
Mwanariadha huyo mlemavu
mwenye umri wa miaka 27, ambaye
hana miguu yake yote mawili,
huenda akahukumiwa jela maisha
iwapo atapatikana na kosa la kuuwa.
Siku ya Jumanne, alilia kizimbani
alipokuwa akielezea yaliyojiri
nyumbani kwake kabla na baada ya
mauwaji hayo.
Iwapo hatapatikana na hatia ya
kukusudia kuua Reeva ,basi
kulingana na sheria za Afrika Kusini,
Pistorious huenda akashtakiwa kwa
kosa la kuua bila ya kukusudia
ambayo hukumu yake ni kati ya
miaka 6- 15 jela.
Mbali na shtaka la mauaji, Pistorius
anakabiliwa na shtaka la kufyatua
bunduki hadharani na shtaka lingine
la kumiliki risasi kinyume na sheria.