PISTORIUS AANDAMWA NA MUONGOZO MASHTAKA WA KESI YAKE


Mwanariadha wa Afrika kusini Oscar
Pistorius amerejea tena mahakamani
kuhojiwa zaidi na kujibu maswali ya
mwendesha mashtaka mkuu Gerrie
Nel katika kesi anayoshtumiwa kwa
kumpiga risasi na kumuua mpenzi
wake mwanamitindo Reeva
Steenkamp nyumbani kwake mwezi
februari tarehe 14 mwaka uliopita .
Bwana Nel amekuwa akimwandama
Pistorius , akisema hakuwa mkweli
katika toba yake na alimfokea
mpenzi wake Reeva Steenkamp mara
kwa mara .
Siku ya kwanza ya maswali ya
mahakama dhidi yake Nel alianza
kwa kuonyesha picha za kutisha za
kichwa kilichochuruzika damu cha Bi
Steenkamp, baada ya kupigwa risasi
na Pistorius.
Mwanariadha huyo anadai
hakumuua makusudi bali alidhani ni
mtu alievamia nyumba yake.
Ameiambia mahakama kuwa
alimpenda sana mwanadada huyo
Reeva .
Kiongozi wa mashataka amemsuta
Pistorious akisema kuwa alikuwa ni
mbinafsi sana kwa mpenzi wake na
kuwa kile alichokijali sana ilikuwa ni
sifa zake na hadhi yake katika jamii.

image

Pistorious alikanusha madai hayo
akisema anajuta kwanini hakuwahi
kumwambia Reeva kuwa anampenda
kupitia ujumbe wa simu ya mkononi.
Pistorius akitoa ushahidi
Mwanariadha huyo alikuwa na
wakati mgumu kuelezea mahakama
kwanini Reeva alimlaumu kwa
kumuonea katika moja ya ujumbe wa
simu ya mkononi wa WhatsApp
ambao alimwandikia Oscar”tangu
turejee kutoka cape town
umekuwa ukinionea sana .”
Viongozi wa mashtaka wana imani
kuwa alimuuwa kimakusudi ndani ya
choo chake baada ya kuzozana.
Mwanariadha huyo mlemavu
mwenye umri wa miaka 27, ambaye
hana miguu yake yote mawili,
huenda akahukumiwa jela maisha
iwapo atapatikana na kosa la kuuwa.
Kinyume ya hali ilivyokuwa Siku ya
Jumanne, alipolia kizimbani
alipokuwa akielezea yaliyojiri
nyumbani kwake kabla na baada ya
mauwaji hayo,
leo alionekana mjasirii na mtulivu
akimjibu Kiongozi wa mashataka ya
umma bwana Nel.
Mamake Reeva bi June Steenkamp
amesema kuwa japo aliombwa
msamaha na Oscar moyo wake
haukumsamehe kwani hadi hapo
Oscar hakukiiri alimua bali alisisitiza
kuwa anaomba msamaha kwa
kusababisha kifo chake.

image

.

Bi Steenkamp mahakamani
Bi Steenkamp alishangaa iwapo
Pistoriuos alikuwa anaigiza au la
kwani amekuwa akilia na kutapika
mahakamani .
Katika tukio lingine Oscar alikataa
katakata kuwa alifyatua risasi katika
mkahawa mmoja alipoulizwa na
kiongozi wa Mashtaka bwana Nel.
Pistorious alisema kuwa hakujua
bunduki hiyo ilikuwa na risasi.
Iwapo hatapatikana na hatia ya
kukusudia kuua Reeva ,basi
kulingana na sheria za Afrika Kusini,
Pistorious huenda akashtakiwa kwa
kosa la kuua bila ya kukusudia
ambayo hukumu yake ni kati ya
miaka 6- 15 jela.
Mbali na shtaka la mauaji, Pistorius
anakabiliwa na shtaka la kufyatua
bunduki hadharani na shtaka lingine
la kumiliki risasi kinyume na sheria.