SERIKALI YA TANZANIA YALIFUTIA USAJILI SHIRIKA LA SISI KWA SISI KUTOKANA NA UCHOCHEZI WA MAPENZI YA JINSIA MOJA.


image

Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja
vinapingwa sana katika mataifa ya
Afrika.
Serikali ya Tanzania imefutilia mbali
usajili wa shirika moja lisilokuwa la
kiserikali kwa sababu ya
kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja
katika jamii.
Shirika hilo kwa jina Sisi Kwa Sisi
lilisajiliwa baada ya kudai kuwa
malengo yake yalikuwa ni kusaidia
jamii.
Tanzania imesema imechukua hatua
ya kufutilia mbali usajili wa shirika
hilo kwa kukiuka sheria za nchi na
kwenda kinyume na malengo ya
usajili wake.
Mkurugenzi wa usajili wa mashirika
yasiyo ya Kiserikali nchini Tanzania,
Maseli Katemba, amesema kuwa
shirika hilo la Sisi kwa Sisi limekiuka
malengo yake ya awali ya kuwapa
elimu na misaada ya kifedha
wananchi lakini mambo yakawa
tofauti.
“Baada ya kufuatilia tumegundua
kuwa sasa wanatilia mkazo
kuwasaidia watu wa jinsia moja,”
alisema Bwana Katemba.
Bwana Katemba amesema kuwa
Serikali itaendelea na kuyasaka
makundi mengine kama hayo
ambayo yanaendesha maswala
yaliyo kinyume na sheria za
Tanzania.

Advertisements