U•N YATELEKEZA KAMBI YA WAKIMBIZI SUDAN KUSINI


image

Maji taka yamezagaa katika kambi
ya Umoja wa mataifa ya wakimbizi
Sudan Kusini
Umoja wa mataifa Nchini Sudan
Kusini umejitetea vikali kutokana na
ukosoaji kwamba inawabagua watu
wanaotaabika ndani ya makao yake
makuu katika jiji kuu la Sudan Kusini
Juba.
Wakimbizi hao wamekita kambi
kwenye ofisi za umoja wa mataifa
baada ya kukimbia mapigano kati ya
wanajeshi watiifu kwa Rais Salva Kirr
Mayardit na aliyekuwa makamu
wake Riek Machar.
Mnamo jumatano wiki hii, kundi la
madkatari wasio na mipaka
Medecins Sans Frontieres lilisema
kuwa watu elfu 20 wanaishi katika
hali ya mateso makubwa baada ya
mvua iliyonyesha majuzi na
kusababisha vyoo kufurika na
kuporomoka.
Toby Lanzer, naibu mkuu wa umoja
wa mataifa mjini Juba ameiambia
BBC kuwa wanatamaushwa pia na
hali mbaya ya maisha ya watu hao
waliokimbia mapigano.
Lakini amesema kuwa kambi hiyo ya
muda haikuwa ihudumie idadi kubwa
ya watu.
Aidha amesema kuwa wanafanya kila
wawezalo ili kuboresha sehemu hiyo
mbali na kujaribu kukodisha shamba
lililo maeneo ya nyanda za juu
viungani mwa mji mkuu ili kujenga
kambi nyingine ya muda ya
kuwahudumia watu.
Umoja wa mataifa wawatelekeza
wakimbizi Sudan Kusini
Shirika moja lisilo la kiserikali la
madaktari wayo na mipaka ,
Medecins Sans Frontieres (MSF)
lilitoa picha na habari zilizosimulia
hali mbaya wanayostahimili
wakimbizi wa ndani kwa ndni nchini
Sudan Kusini huku Wafanyikazi wa
shirika la umoja wa mataifa
linalosimamia maswala Sudan
UNMISS likipuzilia mbali masaibu
yao.

image

MSF ilitoa picha ya Kambi hiyo
ambayo inawatu takriban 21,000
wakiishi katika kambi ambayo maji
taka yamezagaa kwote .
Shirika hilo lilitoaushahidi kuwa vyoo
150 vya kambi hiyo vimeporoka na
uchafu umetapakaa ovyo.
Zaidi ya watu milioni moja
wametoroka makwao .
Takriban watu , 803,200 ni wakimbizi
wa ndani kwa ndani huku wengine
254,000 wametorokea nje ya nchi.
Credit: BBC Swahili.

Advertisements