WAKENYA WALIOTEKWA 2011 WAOKOLEWA


image

Wanajeshi wa Kenya waliopo
AMISOM
Wafanyakazi raia wa Kenya wa
mashirika ya misaada ya kibinadamu
ambao walikuwa wametekwa na
wapinaji wa kiislamu wa Al shabaab
mwaka 2011 wameokolewa na
majeshi ya Kenya.
Daniel Njuguna ambaye alikuwa
akifanya kazi katika shirika la
Madaktari wasio na mipaka
Medecins Sans Frontieres MSF na
James Kiarie wa Shirika la Care
International, walichunguzwa afya
zao na walitarajiwa kusafirishwa
kwenda Nairobi.
Awali walikuwa chini ya uangalizi wa
majeshi ya Kenya ambalo lipo
kwenye kikosi cha Umoja wa Afrika
kilichopo nchini Somalia AMISOM.
Kenya ilituma majeshi yake kwenda
nchini Somalia mwaka 2011 kujiunga
na AMISOM kufuatia matukio ya
utekaji nyara yaliyokuwa
yakiendeshwa na wapiganaji wa Al
shabaab katika mipaka ya nchi hiyo
na Somalia.
Majeshi ya AMISOM yakishirikiana
majeshi yale ya serikali ya Somalia
yamekuwa yakiendesha mapambano
dhidi ya wapiganaji wa Al Shabaab
ambao wanafadhiliwa na kundi la
kigaidi la al Qaeda linaloshikilia
maeneo ya kusini na katikati mwa
Somalia.

Advertisements