BEYONCE,TIMBERLAKE NA PHARRELL WAONGOZA KUPANGWA VIPENGELE VINGI KTK BILLBOARD AWARDS


image

Mchakato tayari umeshaanza wa
kutangazwa majina ya wasanii
watakaowania tuzo za Billiboard
ambazo hufanyika kila mwaka.
Wasanii kama vile Justin Timberlake,
Beyonce Knowles na Pharrell
Williams wameongoza kutajwa
katika vinyanganyiro hivyo kushinda
wanamuziki wengine.
Beyonce ndiye anashikilia usukani
kwa upande wa wanawake akitajwa
kuwania vipengele 7 ikiwemo cha
mwimbaji bora wa kike wa R&B,
albamu bora ya Billboard na albamu
bora ya R&B, wakati kwa wanaume
Justin Timberlake ameongoza kwa
kutajwa kuwania tuzo hizo katika
vipengele 11 kupitia albamu yake
(20/20 Experience) ikiwemo tuzo ya
msanii bora, wasanii 100 bora na
muimbaji bora wa kiume wa R&B.
Akifuatiwa na Pharrell Williams
aliyetajwa kuwania vipengele 7
ikiwemo kolabo ya wimbo wa
‘Blurred Lines’ alioshirikishwa na
Robin Thicke pamoja na Rapa T.I
ambao nao pia wametajwa
kushindania vipengele 5. Rihanna
naye hakuachwa nyuma bali
ameteuliwa kuwania vipengele 5
wakati baba yao ‘Jay Z’ akitajwa
katika vipengele vikubwa 4 kupitia
albamu yake mpya ya ‘Magna Carta
Holly Grail’ na kibao alichoshirikiana
na mkewe ‘Queen Bey’ kinachoitwa
”drunk in love”.

Advertisements