PAPA FRANCIS KUWAWEKEA VIKWAZO MAKASISI.


image

Kiongozi wa kanisa katoliki Papa
Francis
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani
Papa Francis, amewaombea radhi
makasisi wa kanisa hilo
waliowakosea watoto kwa
kuwalawiti.
Papa Francis alinukuliwa kupitia
redio ya kanisa hilo mjini Vatican,
akitaja dhuluma za kingono dhidi ya
watoto kama ukosefu wa maadili
miongoni mwa viongozi wa kanisa
na kusema watakaopatikana na hatia
watawekewa vikwazo.
Mwezi jana Papa Francis, alitetea
vikali rekodi ya kanisa katoliki katika
kukabiliana na tatizo la dhuluma za
kingono zinazotendwa na viongozi
wa kanisa.
Ilikuwa baada ya umoja wa Mataifa
kutuhumu kanisa hilo kwa kukosa
kuwachukulia hatua makasisi
watovu wa nidhamu.
Mwaka jana Papa aliunda kamati
maalum ya kuhakikisha waathiriwa
wa dhuluma za kingono wanapata
kusaidiwa, lakini amekosolewa na
baadhi ya waumini wa kanisa kwa
kujikokota katika kutambua athari za
tatizo hilo hasa kisaikolojia kwa
waathiriwa.
Alisema alihisi umuhimu mkubwa wa
kuomba msamaha kwa niaba ya
makasisi waliowalawiti watoto
ingawa alisisitiza kuwa idadi ya
makasisi hao sio kubwa sana
ikilinganishwa na idadi kamili ya
makasisi wa kanisa hilo.
“Hatutapiga hatua yoyote nyuma
kuhusu tatizo hili, vikwazo
vinavyohitajika lazima vitawekwa,”
alisema papa. ”Lazima tuchukue
hatua kuanzia sasa.”
Katika mahojiano mwezi jana, papa
alilalamika kuwa hakuna aliyechukua
hatua kukabiliana na visa vya ulawiti
wa watoto kanisani ingawa kanisa
linashambuliwa na kuambiwa
limegea katika kuchukua hatua.
Kanisa katoliki limekuwa
likituhumiwa kwa kosa la makasisi
kuwadhulumu watoto kingono katika
mengi ya makaisa yake duniani
kutokana na maaskofu kukosa
kuchukua hatua zozote.
source: BBC NEWS