PICHA ZA AJALI YA MAKAMU WA RAIS _ MH.DK MOHAMMED GHALIB BILAL ,KAMANDA KOVA NA MH. MECKY SADICK


Makamu wa rais wa Tanzania, Dk.
Mohammed Ghalib Bilal
amenusurika katika ajali ya ndege
aina ya helikopta iliyotokea katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
wakati walipokuwa wakikagua athari
za mvua katika mkoa wa Dar es
salaam.

image

Pichani ni ndege aliyopata nayo ajali
makamu wa Rais baada ya kuanguka
katika uwanja wa JNIA huku kikosi
cha zimamoto kikijaribu kuzima
moto wa ndege hiyo
Habari zinasema kuwa helikopta hiyo
inayomilikiwa na jeshi la wananchi
wa Tanzania, ilikuwa imebeba watu 4
akiwemo makamu wa rais Dk Bilal,
mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Said Mecky Sadick, kamanda wa
polisi wa kanda maalum Dar es
salaam ‘Suleiman Kova’ pamoja na
mpiga picha wa TBC George
Kasembe.
Helikopta hiyo ilipata ajali wakati
ikianza kuruka hewani lakini
ikashindwa kuendelea kupaa na
kuanguaka. Hakuna mtu aliyepoteza
maisha, zaidi ya kupata majeraha
madogo madogo ambayo waliweza
kupatiwa matibabu.

image

image

Picha na Jamii Forums

One thought on “PICHA ZA AJALI YA MAKAMU WA RAIS _ MH.DK MOHAMMED GHALIB BILAL ,KAMANDA KOVA NA MH. MECKY SADICK

Comments are closed.