TWEET YA JERRY SLAA KUHUSU MAFURIKO


image

image

ni mtizamo wangu, na
nilimfahamisha Mstahiki meya Jerry
Silaa pia: huyu mtu ana bahati sana
kwamba ni Meya wa manispaa
nchini Tanzania, ambapo
ukisahapata uongozi upo huru
kufanya lolote lile- baya au zuri, la
busara au la kipuuzi- pasi kuchelea
matokeo. Laiti huyu mtu angekuwa
Meya wa eneo lolote lile hapa
Uingereza, basi Jumatatu
angekumbana na wito wa kumtaka
aachie ngazi. Ndio, uwepo wake Dar
(Ilala) usingezuwia mafuriko, lakini
sote twatambua kuwa nyakati za
majanga zinahitaji viongozi
kuonyesha uongozi kwa dhati
(showing leadership). Kilichompeleka
Mwanza ni shughuli za kichama,
ambazo ninaamini zingeweza
kusubiri hadi janga linalowasibu
anaowaongoza limeshughulikiwa.
Japo mwanzoni alileta majibu ya
dharau baada ya kusoma ‘tweets’
hizo mbili za mwanzo hapo juu,
lakini akakumbana na hasira za
wananchi wengi ambao
hawakupendezwa na majibu yake.
Lakini kwa vile neno ‘samahani’
halipo kwenye kamusi za wengi wa
viongozi wetu, Mstahiki Meya
‘aliingia mitini’ kimyakimya…na
hajaonekana tena huko twitter hadi
wakati ninaposti bandiko hili.
Swali la msingi: Hivi Katiba Mpya
tunayohangaika kuipata huko
Dodoma itaweza kweli kutengeneza
mazingira yatakayowawezesha
wananchi kuwashughulikia ‘wahuni
wa kisiasa’ (political thugs)? Jeuri
kubwa inayowafanya watawala wetu
kufanya (including kusema) chochote
ni kutochelea matokeo. Na japo
Katiba tuliyo nayo sasa ina sheria
nzuri tu za kumpatia mwananchi kile
anachostahili (kwa maana ya haki
zake), tatizo limebaki katika
usimamizi wa sheria hizo, na pengine
kubwa zaidi, sheria hizo kubaki kama
maandiko tu yasiyoheshimiwa. Je
Katiba Mpya (laiti ikipatikana)
itaheshimiwa?
Finally, ninaamini Mstahiki Meya
Silaa nafsi itamsuta na atakatisha
ziara yake huko Mwanza na
kuungana na wananchi katika
harakati za kukabiliana na athari za
mafuriko Dar (kwa yeye ni Manisapaa
ya Ilala). See, kwenda kumwona
mgonjwa hakumaanishi kutamfanya
aopone bali kwaonyesha kuwa flani
anajali. Kadhalika, tunapokwenda
kwenye misiba haimaanishi kuwa
tutamfufua marehemu, lakini ile tu
kuwafariji wafiwa kunaonyesha kuwa
tunajali. Nam ,Meya Slaa akiwa Illa/
Dar hatozuiwa athari za mafuriko (au
kama alivyosema mwenyewe
“hawezi kzuwia mvua”) lakini
kibanadamu tu anapaswa kuwa na
wahanga wa mafuriko (japo yeye
ana-pick and choose nani anastahili
kuitwa mhanga)
Source: Jamii Folums