HIKI NDICHO ALICHOSEMA MAALIM SEIF SHARRIF HAMAD KUHUSU MUUNGANO.


image

Amekua mmiliki wa vichwa vya
habari kutokana na ripoti mbalimbali
ambazo zimekua zikimnukuu kwa
kudai kutozitaka serikali mbili lakini
leo April 15 2014 amezungumza
kwenye maonyesho ya miaka 50 ya
muungano ya kuzitoa hizi kauli
zifuatazo.
1. ‘Pamoja na milima na mabonde,
muungano huu umedumu miaka 50,
nchi nyingine zilishindwa, l azima
tufanye tathmini hasa ya muungano
wetu, lazima vijana waelimishwe vp
muungano uliundwa, tulianzia vipi’
2. ‘Ukitaka upate maenedeleo,
yatambue mafanikio yako lakini pia
usisahau matatizo yako, ni ni moja..
kufanya vizuri, Sidhani katika
Tanzania kama kuna watu hawataki
muungano, na kama wapo ni
wachache, muungano uendelee ndio
la msingi’
3. ‘ Sio dhambi watu kuwa na fikra
tofauti, sio dhambi hata kidogo kwa
sababu hatuwezi wote kuwa na fikra
aina moja, Wanaotaka serikali moja
wasibezwe, mbili wasibezwe,
wanaotaka tatu na serikali ya
mkataba wasikilizwe pia’
4. ‘ Wako wanaoamini kwamba
matatizo ya muungano yako kwenye
muundo, tuwasikilize wana hoja gani,
Mwaka 1963 Malaysia na
Tanganyika maendeleo ya sehemu
zote hizi yalikua sawa, mwaka 2014
tujiulize, c hangamoto kwetu ni vipi
tutakua na muungano utakaokua ni
chachu ya maendeleo ya haraka,
mambo ya 74 ni tofauti na 2014′
5. ‘Tuwe makini sana, sote ni wa
nchi moja, tujiepushe na kikundi
chochote kuona wao wana haki zaidi,
Watanzania wote sawa, wajumbe wa
bunge maalum waangalie maslahi ya
nchi, muungano huu ni wa nchi 2
zilizokua dola huru na kuungana kwa
hiari’
6. ‘ Tupate katiba ambayo itaondoa
migogoro, kero iwe ni historia… hili
swala lisiwepo tena, t usiende kwenye
maamuzi ya harahaharaka tukasema
serikali mbili au tatu bila kuangalia
athari zake, k atiba ya Znz inasema ni
miongoni mwa nchi mbili za
muungano, ya Muungano inasema
Tz ni nchi moja, huo ni mgogoro’
7. ‘ Nadhani Warioba
walivyopendekezwa waliona hisia za
Znz zilivyo, tunataka katiba
itakayotambua usawa wa nchi mbili,
h akuwezi kuwa na katiba ambayo
itamridhisha kila mtu lakini angalau
wengi wao waridhike’