INDIA KUTAMBUA WALIOBADILISHA JINSIA


image

India ina karibu watu milioni mbili
waliobadilisha jinsia yao kutokana
na hisia zao
Mahakama ya juu zaidi nchini India
imetoa uamuzi wa kihistoria
unaotambua watu waliobadilisha
jinsia yao kama watu wa kawaida
katika jamii.
Kawaida kuna jinsia mbili, mke au
mume lakini mahakama hiyo
imesema kuwa watu wanaoamua
kubadilisha jinsia yao kuambatana
na hisia zao pia ni lazima
watambuliwe na jamii na walio
katika aina ya jinsia kivyao.
Mfano wa watu kama hao ni mtu
anayezaliwa kama mwanamke lakini
anahisi kisaokolojia kuwa yeye ni
mwanaume na hivyo hubadilisha
jinsia yake na kuwa mwanamume
kwa hata kufanyiwa upasuaji.
Uamuzi huu wa mahakama bila
shaka ni wa kihistoria na unasema
watu hao wasio jitambua kama
wanaume au wanawake
wanaruhisiwe na kutambulika kama
wanavyotaka
Katika kitambulisho chao
hawatajulikana kama wanaume au
wanawake bali ‘Transgender’ kama
jinsia ya tatu, sio wanaume wala
wanawake.
“ni haki ya kila binadamu, kuchagua
jinsia wanayoitaka,” alisema jaji
katika uamuzi huo ambao unawapa
watu hao haki ya kujitambulisha
kama wanaume au wanawake
Iliamuru serikali kuwapa watu hao
nafasi za kazi na elimu kama jamii
ya watu waliotengwa. Mahakama pia
imeitaka serikali kuwapa huduma
muhimu watu hao wanaochagua
kujitambulisha watakavyo.
Takwimu zinasema kuwa watu
milioni mbili nchini India
wamebadilisha jinsia yao.
Wanaharakati wanasema kwamba,
watu hao wanatengwa na kuishi
katika umaskini mkubwa na pia
wanachukiwa kwa sababu ya
kubadilisha jinsia yao.
Wengi hujikimu kimaisha kwa kuwa
waimbaji , kuombaomba barabarani
na kujihusisha na biashara ya ngono.
Kadhalika wanaharakati wanasema
kuwa watu hao hunyimwa huduma
za matibabu hospitalini.
”Watu hawa ni raia wa India na
lazima waheshimiwe na kupewa
nafasi ya kunawiri maishani,”
alisema jaji katika uamuzi wake.
“lengo la katiba ni kuhakikisha kila
mtu wa India anapewa nafasi ya
kuishi vyema na kujiendeleza
maishani, licha ya jinsia , dini na
jamii anakotoka”

Advertisements