OSCAR PISTORIUS AMALIZA KUJITETEA


image

Oscar Pistorius anakana kumuua
mpenzi wake Reeva Steenkamp
Upande wa mashitaka katika kesi ya
mauaji dhidi ya Oscar Pistorius
umemaliza kumhoji mwanariadha
huyo.
Oscar aliyekatwa miguu yote miwili
anakana kutekeleza mauaji hayo
akisisitiza kwamba alidhani
marehemu Steenkamp alikuwa
jambazi aliyevamia nyumba mwake.
Anakabiliwa na kifungo cha kati ya
miaka 25 au maisha gerezani, iwapo
atapatikana na makosa ya mauaji ya
kupangwa.
Kabla ya kuanza kusikizwa kesi hiyo,
mwendesha mashitaka Gerrie Nel
alisema kuwa alitumai kumaliza
kumhoji mwanariadha huyo siku ya
Jumanne.
Alimuomba Jaji Masipa aahirishe
kesi wakati wa mapumziko ya
pasaka hadi tarehe 5 Mei.
Ameeeleza kwamba mawakili
wenzake wanakabiliwa na kesi
nyengine ‘nzito zaidi’ wanazostahili
kuzishughulikia pamoja na ‘masuala
ya kibinafsi’.

image

Pistorius akitoka mahakamani
Ombi hilo liliungwa mkono na
upande wa utetezi, uliosema
kwamba kesi hiyo inapaswa
kumalizika tarehe 16 Mei kama
ilivyopangwa. Jaji alisema atatoa
hukumu yake ya ombi hilo siku ya
Jumatano.
Siku ya Jumatatu, Bwana Nel
alipendekeza kwamba Pistorius
anajifanya kuzidiwa na hisia kuficha
matatizo anayopata kujibu masuali
mazito anayoulizwa.
Jaji Thokozile Masipa alisitisha kwa
muda kesi hiyo mara mbili siku ya
Jumatatu baada ya Pistorius kuanza
kulia.
Muda mfupi kabla kesi kumalizika
kwa siku, Nel alisema: ” unazidiwa
na hisia sasa kwa sababu unaudhika,
kutokana na kuwa ushahidi wako
huenda si wa kweli.”
Mwendesha mashtaka huyo
anayejulikana kwa mtindo wake wa
kutishia watu anapowahoji, baadaye
alimuuliza Pistorius: ” Hautumii hisia
zako kukwepa kujibu maswali?”
Pistorius alisema akili yake
haikumanika kama inavyostahili
wakati wa ufyetuaji risasi huo.
Upande wa mashitaka umesema,
kuwa Pistorius anatumia machozi
yake kama sababy ya kutaka
kuhurumiwa
Awali, kwa mara nyengine Nel
alimdadisi kwa uzito Pistorius
kuhusu wakati alipompiga Bi
Steenkamp risasi.
Mwanariadha huyo alisisitiza
kwamba hakuna na nia ya kumuua
mtu yoyote, alisema: “Nilifyetua
risasi kutokana na uoga.”
Nel baadaye alisema kwamba
Pistorius alibadili ushahidi wake
kutoka kusema alikuwa akijikinga na
hadi kusema kwamba alifyetua risasi
kwa makosa.
Mwendesha mashtaka akasema hii
ni kutokana na kuwa ukweli ni :
“Ulimfyetulia Reeva risasi.”
“Sio kweli,” Pistorius akajibu, huku
akibubujikwa kwa machozi na
kuilazimu mahakama kusitisha
vikao kwa muda.
Pistorius alisema yeye na marehemu
Steenkamp walibarizi jioni pamoja
kabla ashutuke usingizini kutokana
na kusikia sauti iliyotoka bafuni.
Mashahidi wa upande wa mashitaka
walieleza kusikia mwanamke
aliyepiga mayowe, lakini upande wa
utetezi unakana ushahidi huo.
Source: BBC  & TVC

4 thoughts on “OSCAR PISTORIUS AMALIZA KUJITETEA

Comments are closed.