RAPPER 50¢ @50cent ATAKIWA KULIPA MAMILLION YA DOLLARS KWA KAMPUNI YA SLEEK AUDIO


image

Wote tunafahamu kwamba rapper 50
cent anajua kutumia fursa za kuweza
kujitengenezea fedha. Lakini safari hii
biashara zake zimemletea matatizo
kupitia kesi iliyodumu kwa miaka 3
kati yake dhidi ya kampuni ya
kutengeneza earphone – Bradenton.
Kwa mujibu wa mtandao wa
http://www.hot97.com, ni kwamba 50 Cent
ameamriwa na mahakama kuilipa
kampuni hiyo kupitia kitengo chake
Sleek Audio karibia $4.5 million
kama fidia ya malipo mwanasheria
na $11.7 million kama fidia ya
kuvunjika kwa mkataba na kampuni
hiyo ambayo ilikuwa wakishirikiana
kutengeneza 50 Cent headphones.
50 Cent mwanzoni alituhumiwa
kuiba designs za Sleek Audio,
ambazo mwanzoni alipewa kwa ajili
kuzipitisha kwa ajili ya kuanza kwa
uzalishaji wa headphones hizo, lakini
baadae 50 aliwageuka Sleek na
akaamua kushirikiana na kampuni
nyingine kutumia designs alizopewa
na kampuni ya Sleek.

Advertisements