UINGEREZA YAPIGA MARUFUKU WANAUME KUTEMBEA VIFUA WAZI.


image

‘Sio kila mtu anavutiwa na vifua
wazi’
Wanaume wanaovua mashati
wamepigwa marufuku kuitembelea
bustani ya mapumziko na kujivinjari
ya Adventure Island.
Ni eneo ambalo watu wanakwenda
kujivinjari na familia zao, kwa
kutazama wanyama, watoto hupata
kubembea na pia watu huota jua.
Bustani hiyo iliyopo mjini Southend
nchini Uingereza, imeweka ilani
zinazowaomba wanaume wasivue
mashati yao, na kwamba watakao
patikana watafukuzwa.
Mkurugenzi mkuu, Marc Miller,
amesema anataka wanaume
waonyeshe “ustaarabu”.

image

Adventure Island inasema
imeidhinisha marufuku hiyo kuzivutia
familia
Bustani hiyo inasifika duniani kwa
kuwa na idadi kubwa ya watu walio
uchi walioipanda bembea ya
‘Rollercoaster’ – licha ya kwamba ni
jambo linalofanyika faraghani.
‘Kuilenga Familia’
Zaidi ya watu 100 walivua nguo ili
kuipanda bembea hiyo ijulikanayo
kama Green Scream mnamo 2010.
Miller anasema: “Katika miaka ya
hivi karibuni, tumekuwa tukiongeza
idadi ya vijana na wanaume ambao
huvua mashati yao ili kupata joto la
jua kwa wingi. Hilo ni sawa kabisa
lakini katika mazingira yanayofaa”.
“Tunajaribu sana kufanya biashara
inayoivutia familia na sio kila mtu
anavutiwa kuona vifua wazi”.
Pamoja na kuwa na idadi kubwa
duniani ya watu wasio vaa nguo,
Adventure Island pia ilijaribu kuweka
rekodi mpya ya kuwa na watu wengi
wanaocheza mpira wa gofu wakiwa
uchi, mnamo mwaka 2012.
Msemaji mmoja anasema michezo
yote hufanyika faraghani.
“Wanaohudhuria michezo hiyo ni
waliojisajili kushiriki, ili kuchanga
fedha nyingi za misaada ya
kukabiliana na magonjwa kama
saratani ya matiti na ya uume,”
alisema.
“Marufuku hiyo imetolewa wakati
bustani imefunguliwa kwa umma.”

One thought on “UINGEREZA YAPIGA MARUFUKU WANAUME KUTEMBEA VIFUA WAZI.

Comments are closed.