FERRY MOJA YAZAMA KOREA


image

Ferry yenye abiria 460 ikizama Korea
Kusini.
Oparesheni ya uokozi inaendelea
kufuatia ishara za dharura
zilizoripotiwa kutoka meli moja
ilioyobeba takriban abiria 460 katika
pwani ya Korea Kusini.
Maafisa wanasema kuwa walinzi wa
pwani hiyo, meli za wanamaji wa
Korea pamoja na ndege za uokoaji ,
zimepelekwa katika ferry moja
inayozama kusini mwa pwani hiyo.
Shughuli zinaendelea hivi sasa
kuokoa zaidi ya abiria 460 wa ferry
hiyo .
Jeshi la wanamaji likishirikiana na
maafisa wanaolinda usalama katika
bahari ya rasi ya Korea.
Maafisa wanasema walipokea habari
kuwa meli hiyo imepata matatizo
ikiwa imebeba idadi kubwa ya
wanafunzi ikitoka Incheon iliyoko
kwenye visiwa vya kifahari vya Jeju .
Waokoaji wamewanusuru tayari
abiria 160 huku wengine waliosalia
wakishauriwa waruke baharini
iliwaokolewe.
Walioshuhudia wanasema kulisikika
kishindo kikubwa kabla ya ferry hiyo
kuanza kusakama maji zaidi ya
kilomita 20 kutoka ufukweni.
Shughuli ya uokoaji bado inaendelea
huku duru zikidhibitisha kuwa mtu
mmoja amepatikana ameaga dunia.

Advertisements