Mvinyo wamtia mashakani kiongozi Australia


image

Barry O’Farrell amekiri kuwa alikosa
kwa kutosema ukwlei ingawa
alighafilika
Kiongozi wa jimbo lenye idadi kubwa
ya watu nchini Australia,New South
Wales, amejiuzulu baada ya kukosa
kutangaza kuwa alipata zawadi ya
mvinyo yenye thamani ya dola 2,800.
Waziri mkuu wa New South
Wales ,Barry O’Farrell alikiri kuwa
alisahau au alighafilika kwa bahati
mbaya baada ya kuambia jopo moja
linalochunguza visa vya ufisadi kuwa
hakuwahi kupokea mvinyo wowote
kutoka kwa mtu yeyote.
Bwana O’Farrell, alisema hangeweza
kukumbuka kumpigia simu
mfanyabiashara Nick Di Girolamo,
aliyemkabidhi zawadi ya mvinyo
mwaka 2011.
‘hakukumbuka kamwe ‘
O’Farrell, ambaye ni kiongozi wa
chama cha Liberal, katika jimbo la
New South Wales, alitangaza
kujiuzulu mjini Sydney Jumatano.
Aliambia wandishi wa habari
kwamba haikuwa nia yake
kulipotosha jopo hilo.
“nakubali kuwa kuna ujumbe wa
shukrani nilioutia saini na kama mtu
ambaye anaamini katika uwajibikaji,
ninakiri makosa yangu, ” alisema
O’Farrell.
Aliongeza kuwa waziri mkuu mpya
wa jimbo hilo atachaguliwa katika
kikao cha bunge wiki ijayo.
“siwezi kueleza kwa kweli ikiwa
ilikuwa zawadi na nilivyoipata,”
alisema waziri mkuu huyo.”Lakini
nakiri kosa langu.”
Waziri mkuu wa Australia Tony
Abbott, amesema kuwa kujiuzulu
kwa bwana O’Farrell, ilikuwa ishara
ya maadili mema wala sio ufisadi.
Amemtetea akisema kuwa
alighafilika kweli wala hakunuia
kusema uongo kwa maksudi

Advertisements