Nay wa Mitego aingia mkataba mnono na kampuni ya simu


Msanii wa Hip Hop, Nay Wa Mitego
amepata deal la matangazo na
kampuni ya simu itakayomlipa zaidi
ya shilingi billion 70

image

kuwa mkataba aliosaini utakuwa
wazi mwezi ujao.
“Nimeingia mkataba na kampuni ya
simu sio kama balozi ni mtu ambaye
atakuwa anatumika katika
matangazo yao na vitu vingine kwa
kipindi cha mwaka mzima,”
amesema. “So nafikiri watu
wasubirie tarehe moja nitaanza kazi
rasmi ndipo nitakuwa huru
kuzungumzia mkataba wangu.
Mkataba wangu ulikuwa na vikao
vingi huku na kule ili kutafuta
maslahi, ila namshukuru tumefika
makubaliano mazuri nimesaini
mkataba wa mwaka mmoja. Naweza
sema utanipa pesa nyingi sana huu
mkataba, kwasababu utabadilisha
baadhi ya viwango vyangu vya
show,hata ubora wa kazi zangu,
kwahiyo kwangu naweza sema ni
hatua muhimu sana. Siwezi leo
kuzungumzia kiasi ambacho nitapata
ila tambua ni mkataba mzuri sana,ni
zaidi ya shilingi milioni 70. Nadhani
nitaitamka rasmi baada ya kuanza
kazi tarehe moja ninaweza
kuzungumza mambo mengi kuhusu
mkataba wangu.”
SOURCE: BONGO5

Advertisements