UFALME WA BUGANDA WAREJESHEWA MALI.


image

Ronald Kabaka Mutebi wa pili ndio
mfalme wa Buganda
Rais wa Uganda Yoweri
Museveni,amemkabidhi mfalme wa
Buganda mali ambayo ufalme huo
ulipokonywa mnamo miaka ya sitini.
Mali hiyo ambayo ni pamoja na
ardhi, majumba na hati za kumiliki
ardhi ilikabidhiwa kwa mflame wa
Buganda katika sherehe iliyofanywa
mjini Kampala.
Buganda ndio ufamle mkubwa wa
kitamaduni uliosalia nchini humo.
Ulifutiliwa mbali na aliyekuwa Rais
Milton Obote mwaka 1966 lakini
ukarejeshwa tena na Rais Museveni
mapema miaka ya tisini.
Rais Museveni alikabidhi nyaraka za
umiliki wa mali hiyo kwa naibu mkuu
wa Katikiro au waziri mkuu wa
ufalme huo Emmanuel Sendaula
katika hafla iliyofanyika katika Ikulu
ya Rais mjini Entebbe.
Kadhalika Rais Museveni alisifu
ushirikiano uliopo kati ya utawala wa
Kabaka na serikali.
Museveni aliongeza kuwa uhusiano
kati ya pande hizo mbili utasalia
kuwa mzuri na kwamba vizingiti
vilivyokuwepo vimeondolewa na
kuwa Rais hataki mzozo wa kijamii.
Alisema Kabaka Ronald Mutebi wa
pili, anaweza kuzuru Kayunga bila
wasiwasi wowote.

Advertisements