Waisilamu hawatapelelezwa tena New York


image

Kamishna wa polisi New York
William Bratton alikutana na
wakereketwa wa mpango huo
Idara ya polisi mjini New York
Marekani, imefunga kitengo chake
maalum cha ujasusi ambacho
huwapepeleza waisilamu ili
kuchunguza kama kuna tisho lolote
la ugaidi.
Kitengo hicho kilikuwa kinatumia
polisi waliokuwa wanavalia nguo za
kiraia kusikiliza kisiri mawasiliano ya
simu kati ya waisilamu na hata
kuzuru maeneo yanayotembelewa
sana na waisilamu.
Vyombo vya habari nchini Marekani
vinasema kuwa kitengo hicho
kiliwahi kushitakiwa mara mbili kwa
mbinu zao za ujasusi na pia
kulaaniwa na makundi ya
wanaharakati wa haki za binadamu.
Pia kiliwaghadhabisha waisilamu
hasa kwa kuwachunguza.
“mageuzi haya ni hatua muhimu
sana katika kuondoa hali ya
wasiwasi na kutoaminiana kati ya
polisi na jamii ili jamii iweze
kusaidia polisi kuwashika wahalifu,”
ilisema taarifa kutoka katika ofisi ya
meya wa New York Bill de Blasio.
‘Vita vya kisaikolojia’
Hatua ya kusitisha mpango huo,
ilifikiwa na kamishna mpya wa polisi
wa kituo hicho, na inaonekana kama
njia moja ya kubadili mbinu za
kukusanya ujasusi ambazo wengi
wanasema zilichangia mashambulizi
ya Septemba 9/11
Kitengo hicho, kilichoanzishwa
mwaka 2003, na baadaye kuitwa, ‘
Zone Assessment Unit ‘ kilipeleleza
waisilamu hasa maeneo walikofanya
kazi, kuswali, kununua madukani na
hata mikahwa walikokuwa
wanakulia.
Wakuu wa kitengo hicho wanasema
kuwa kazi yao iliathiri sana uhusiano
kati ya jamii na polisi

Advertisements