WATU WATATU WANAODHANIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAVAMIA BENKI YA BARCLAYS.


image

Dar es salaam, Tanzania. Watu
watatu wanodhaniwa kuwa ni
majambazi wakiwa na pikipiki aina
ya Boxer na silaha za moto, waliingia
ndani katika benki ya Barclays tawi
la Kinondoni majira ya saa 3 asubuhi
na kufanikiwa kuiba fedha ambayo
kiasi kamili hakijafahamika hadi
sasa.
Baadhi ya wakazi wa jiji waliokuwa
katika eneo hilo wameshauri jeshi la
polisi kanda maalum ya Dar es
salaam kuhakikisha kuwa benki zote
jijini na nchini zinalindwa na askari
polisi ambao watakuwa na silaha za
moto tofauti na makampuni ya watu
binafsi ambao askari wake
wanakuwa hawana silaha bali ni
virungu.
”Hakuna sabbau ya kuwa na walinzi
kabisa, afadhali serikali na jeshi la
polisi wajipange kuchukua nafasi
hizo. alisema mkazi mmoja wa jijini
Dar es salaam

Advertisements