Double Impact: Jay Z na Beyonce kufanya ziara ya muziki ya pamoja kuanzia June 2014


Jay Z na Beyonce kwenye ziara
moja? Patakuwa hapatoshi. Kwa
mujibu wa ripoti, wanandoa hao na
wazazi wa Blue Ivy watakuwa na
ziara ya Marekani.

image

Mtandao wa Page Six umeandika
kuwa wapenzi hao wenye nguvu
duniani wapo mbioni kutangaza ziara
ya viwanjani ambapo watatumbuiza
pamoja kwenye viwanja vikubwa 20
nchini Marekani. Wakati ambapo
bado tarehe rasmi ya ziara hiyo
haijatangazwa, inadaiwa kuwa
inaweza kuanza June na huenda
wakawa na show jijini New York, July
4.
Wawili hao wameliza ziara zao
binafsi hivi karibuni ambapo Jay Z
alimalizia ziara ya show 52 ya
‘Magna Carta…Holy Grail’ mwezi
January, wakati Beyonce akimaliza
yake ya ‘Mrs. Carter Show’ mwezi
March.