Forbes yatoa orodha ya wasanii 5 wa Hip Hop matajiri zaidi 2014, Diddy awashinda Jay Z, Dre na 50 Cent


Forbes imetoa orodha ya wasanii
wasanii watano wa Hip Hop matajiri
zaidi 2014. Sean “Diddy” Combs ,
zamani Puff Daddy au P Diddy na
sasa Diddy ndiye anayeongoza katika
orodha hiyo kwa kuwa msanii tajiri
zaidi wa Hip Hop 2014 kwa mujibu
wa Forbes.

image

Utajiri wa Diddy unakadiriwa kuwa
dola milioni 700, ikiwa imeongezeka
dola milioni 120 kutoka mwaka jana
huku vyanzo vya utajiri wake
vikitajwa kuwa ni Revolt TV/Diageo’s
Ciroc.
Anayefuatia katika nafasi ya pili ni
producer Andre Young aka Dr. Dre
ambaye ana utajiri unaofikia dola
milioni 550. Utajiri wake umetokana
na mauzo ya headphones za Beats
by Dr. Dre.
Nafasi ya tatu imeshikwa na Shawan
Carter aka Jay Z, kwa utajiri wa dola
milioni 520 huku vyanzo vya utajiri
huo vikitajwa kuwa Rocawear Sale/
Live Nation/Roc Nation.
Nafasi ya nne imekamatwa na Bryan
Williams aka Birdman, huku utajiri
wake ukitokana na Cash Money/
YMCMB/GT Vodka.
Wa mwisho katika orodha hiyo
aliyeshika nafasi ya tano ni Curtis
Jackson aka 50 Cent, mwenye utajiri
wa dola miliono 140, vyanzo vyake
vikitajwa kuwa ni Vitamin Water/
SMS Audio/SK Energy.
Story hii ni sehemu ya story
itakayotoka katika jarida la Forbes la
May 5.
The Forbes Five: Hip-Hop’s
Wealthiest Artists 2014
1.Sean “Diddy” Combs | $700 Million
| Revolt TV/Diageo’s Ciroc
2.Andre “Dr. Dre” Young” | $550
Million | Beats by Dr. Dre Headphones
3.Shawn “Jay Z” Carter | $ 520
Million | Rocawear Sale/Live Nation/
Roc Nation
4.Bryan “Birdman” Williams | Cash
Money/YMCMB/GT Vodka
5.Story kamili ya orodha hii itatoka
katika toleo la May la jarida la
Forbes.
Source: BONGO5. &FORBES MAGAZINE. 

Advertisements