Nigeria:Wazazi wawasaka watoto msituni


image

Shule ya mabweni iliyovamiwa huku
wasichana zaidi ya miamoja
wakitekwa nyara
Wazazi wa takriban watoto miamoja
waliotekwa nyara na watu
wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa
kundi la Boko Haram wameingia
msituni kuwatafuta watoto wao.
Wasichana hao walitekwa nyara
kutoka shuleni mwao katika eneo
moja la vijijini Kaskazini Mashariki
mwa Nigeria Jumatatu usiku.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria
anasema kuwa ni hatari sana kwa
wazazi hao hata kutafakari kuingia
msituni , kwani wapiganaji wa Boko
Haram wamewaua mamia ya watu
mwaka huu , kwa kuwakata vichwa
vyao.
Rais Goodluck Jonathan, anakutana
na magavana wa majimbo na
maafisa wakuu wa jeshi kujadili
swala la usalama.
Awali jeshi lilisema ni wasichana 18
pekee kati ya 129 waliotekwa nyara
bado hawajapatikana .
Wengine wote walifanikiwa kutoroka
kutoka mikononi mwa Boko Haram.
Lakini wazazi wanapinga kauli ya
jeshi na wanasema kuwa wasichana
wengi bado hawajulikani waliko.
Wapiganaji hao waliwateka nyara
wasichana kutoka shule ya wabweni
walipokuwa wanajiandaa kwa
mitihani yao.
Duru zinasema ni wasichana 17
pekee waliofanikiwa kutoroka
kinyume na kauli ya jeshi.
Inaanimika kuwa wapiganaji wa
Boko Haram ndio wamewateka nyara
wasichana hao na kuwapeleka katika
msitu ulio karibu na mpaka wa
Nigeria na Cameroon.
Kundi hilo linapiga vita serikali ya
Nigeria likisema kuwa linataka nchi
hiyo itawaliwe kwa misingi ya
kiisilamu.
Jumatano watu 18 waliuawa katika
shambulizi lililofanywa wilayani
Gwoza Kaskazini Mashariki mwa
Nigeria.
Wadadisi wanasema shambulizi
dhidi ya wasichana ni jambo la aibu
kubwa kwa serikali
Taarifa ya jeshi ilisema kuwa
wasichana wengi walifanikiwa
kutoroka ingawa wazazi wanakana
madai hayo wakisisitiza kuwa
wasichana wengi bado
hawajapatikana

Advertisements