Rais Bouteflika kugombea Urais Algeria


image

Rais Bouteflika anaugua kiharusi
Wananchi wa Algeria leo wanapiga
kura kumchagua Rais mpya. Rais wa
sasa Abdelaziz Bouteflika anawania
kwa muhula wa nne.
Bwana Bouteflika, mwenye umri wa
miaka 77, hajaonekana sana
hadharani tangu kupatwa na kiharusi
mwaka jana.
Pia hajaonekana akifanya kampeini
zake hadharani.
Uchaguzi huo unashirkisha
wagombea sita.
Upinzani umefanya maandamano ya
kuupinga uchaguzi huo na kuwataka
watu kuasusia wakiutaja kama kiini
macho.
Wanasema kuwa Bouteflika hana
uwezo wa kugombea kwa sababu ya
afya yake mbaya.