Iyanya adai kulipwa tshs mil 6.5 na suti mpya kuonekana kwenye video ya Habida


Muimbaji wa Nigeria, Iyanya
ameombwa alipwe kiasi kikubwa cha
fedha kutokea kwenye video ya
wimbo alioshirikishwa na msanii wa
Kenya, Habida.

image

Habida amedai kuwa uongozi wa
Iyanya umedai ulipwe $4000 ambazo
ni zaidi ya shilingi milioni 6.5 ili
kuonekana kwenye video hiyo.
Pia walitaka Habida amnunulie
Iyanya suti mpya ya kuvaa kwenye
video hiyo.
Kama hiyo haitoshi, walitaka msanii
wa mitindo binafsi na ukijumlisha
vyote hivyo zaidi ya shilingi milioni 9
ilikuwa inahitajika.
“Sina uhakika kama Iyanya alikuwa
anajua kinachoendelea. Sikuweza
kutimiza matakwa hayo kwa muda
huo na nimeamua kuutoa wimbo huo
mapema,” Habida aliiambia Heads
Up ya Kenya.
Source: BONGO5

Advertisements