RAPA ANDRE JOHNSON WA WU- TANG CLAN AFYEKA NYETI ZAKE.


image

Hii ndio Dunia, ukistaajabu ya Musa
utayaona ya firauni. Rapa aliyepata
umaarufu kupitia kundi la Wu-Tang
Clan ‘Andre Johnson’ AKA Christ
Bearer amenusurika kupoteza maisha
baada kuukata uume wake kwa kisu
na kisha kujirusha ghorofani.
Tukio hilo lilitokea Jumatano majira
ya asubuhi katika jengo la North
Hollywood, huku taarifa za polisi
zikidai kwamba, licha ya kukata
sehemu zake nyeti alipatwa na
majeraha kadhaa mwilini mwake hali
iliyopelekea akimbizwe katika
hospitali ya Sinai kwa kile
kilichodaiwa ni jaribio la kutaka
kujiua.
Kwa sasa Johnson anapatiwa
matibabu hospitalini hapo ingawa
bado haijaweza kufahamika sababu
ya yeye kufanya kitendo hicho. Tukio
hilo limetokea ikiwa ni siku moja
kupita tangu video ya wimbo wake
wa Ooooh! aliomshirikisha Rugged
Mork kuwekwa katika mtandao wa
YouTube.

image

Advertisements