WALIOPOTEZA NDUGU ZAO KWENYE KIVUKO CHA SOWEL WAMCHENJIA NAHODHA WA MELI HIYO.


image

Juhudi za kukoa watu waliozama
kwenye kivuko cha Sowel, Korea
Kusini bado zinaendelea huku watu
waliopoteza ndugu na jamaa zao
wakimjia juu kiasi cha kutaka kumpa
kichapo nahodha wa ferry hiyo ‘Lee
Joon-Seok’.
Miongoni mwa abiria 475 na
wafanyakazi wa kivuko hicho ni watu
179 pekee ndio waliookolewa na
wengine 271 hawajulikani walipo
hadi hivi sasa.
Serikali ya Korea kusini imeendelea
na utafutaji wawatu waliosalia kwa
kutumia nyambizi kukipekua kivuko
hicho kilichozama . Wapiga mbizi
wamekuwa wakikabiliana na upepo
mkali pamoja na mawimbi kujaribu
kukifikia chombo hicho.

image

Mashua moja ya wavuvi iliweza
kuwaokoa watu watatu ambao
walikuwa wanapelekwa na maji
ingawa kuna taarifa zinazosema
kuwa chombo hicho kilikwenda
mrama licha ya abiria kuhoji
mchango wa nahodha wake ambaye
aliomba radhi kituo cha polisi na
kudai kufedheheshwa na tukio hilo.
Katika mkusanyiko mmoja wa
jamaa, bibi aliyempoteza mjukuu
wake aliomba dua ili mjukuu huyo
aweze kupatikana, ”Uko wapi Jing
Yong nategemea urejee nyumbani
pamoja na mama yako na baba yako
ukiwa mzima”.

Advertisements