Mbunge auawa na Al Shabaab Mogadishu


image

Gari ambalo lilikuwa na bomu
lililokuwa limetegwa na Al Shabaab
Mbunge mmoja ameuawa katika
shambulizi la bomu lililokuwa
limetegwa ndani ya gari mjini
Mogadishu Somalia.
Kundi la wanagmabo la Al Shabaab
limekiri kufanya shambulizi hilo dhidi
ya mbunge Isak Mohamed Rino.
Mbunge mwingine Mohamed Ali,
alijeruhiwa katika shambulizi hilo
ambalo limetokea huku serikali ikiwa
mwenyeji wa kongamano la
usalama.
Wanajeshi wa serikali wameweza
kupiga hatua dhidi ya wapiganaji wa
al-Shabaab katika siku za hivi
karibuni , lakini kundi hilo bado
linadhibiti maeneo mengi ya Kusini
mwa Somalia.
Waziri mkuu Abdiweli Sheikh Ahmed,
amelaani shambulizi hilo na kulitaja
kama kitendo cha uoga.
Rais Hassan Sheikh Mohamud
mnamo siku ya Jumapili, alifungua
rasmi kongamano hilo akisema kuwa
tabia ya mashambulizi ya kiholela
ambayo yamegubika Somalia kwa
miaka 23 lazima ikome.
Kundi la Al-Shabaab hufanya
mashambulizi ya mara kwa mara ya
kuvizia mjini Mogadishu na katika
maeneo mengine ya nchi hiyo.
Somalia imekuwa ikikumbwa na vita
vya wenyewe kwa wenyewe tangu
mwaka 1991 wakati Siad Barre
alipopinduliwa.

Advertisements