Rais wa Korea Kusini alaumu nahodha


image

Juhudi za uokozi zingali zinaendelea
Rais wa Korea kusini Park Geun Hye
amemkosoa nahodha na wafanyikazi
wa Feri ya abiria iliozama kwa
kuikimbia feri hiyo na hivyobasi
kufananisha vitendo vyao na mauaji.
Matamshi ya rais Park yanafuatia
uchapishaji wa mawasiliano kati ya
feri hiyo na waokozi ,yaliobaini
kwamba kulikuwa na hali ya
wasiwasi mbali na kutokuwepo
mpangilio wa uokozi.
Idadi ya watu waliofariki
imeongezeka na kufikia 64 huku watu
238 wakiwa hawajulikani
waliko,wengi wao wakiwa wanafunzi
wa shule.
Wapiga mbizi wanaendelea na juhudi
za kutafuta mili ya watu waliozama
na feri hiyo huku wakijitahidi kuingia
ndani ya feri yenyewe.
Habari zilizotangazwa kuhusu
mawasiliano ya mwisho kati ya
wafanyakazi wa Feri iliyozama Korea
Kusini na maafisa wa kudumisha
usalama baharini zinaonyesha kuwa
kulitokea hali ya wasiwasi kabla ya
mkasa huo, ambayo huenda
ilichangia pakubwa vifo vya abiria
wengi katika feri hiyo.
Taarifa hiyo mpya ilitolewa Jumapili
alasiri wakati ambapo
imethibitishwa kuwa maiti 62
zimepatikana kwenye mabaki ya feri
hiyo, na kufanya idadi ya watu
waliothibitishwa kufariki kufikia 58.
Zaidi ya watu 240 hawajulikani
waliko hivi sasa.

image

Jamaa wa waathiriwa walikabiliana
na polisi wakilaumu waokozi kwa
kujikokota
Jamii za watu ambao hawakuwa
wamepatikana walifanya maombi ya
Pasaka Jumapili katika chumba cha
kufanyia mazoezi katika eneo la
Jindo, ambako mamia ya watu
wamekusanyika tangu feri hiyo
kupinduka wakisubiri habari
kuwahusu wapendwa wao.
Mama mmoja alisema kuwa watoto
waliofariki walikuwa wakitunzwa
vizuri.
“Naamini watoto hao wako
mbinguni ,” mama huyo alisema.
Jung Maria, mwanamke aliyejitolea
kuzisaidia familia za walioathirika,
alisema kuwa jamaa za watu
wasiojulikana waliko wanapaswa
kusikia kilichotokea kwa njia moja au
nyingine.
“ikiwa wamefariki, tunapaswa kupata
miili yao haraka iwezekanavyo. Na
iwapo kutatokea muujiza basi
turejeshewe watoto hao upesi pia,
alisema mfanyakazi huyo wa
kujitolea
Idadi kubwa ya abiria katika meli hiyo
walikuwa wanafunzi wa shule ya
upili waliokuwa wakienda kwenye
mojawapo wa kisiwa kubarizi. Hadi
kufikia sasa kumekuwa kungali kuna
ubishi mkubwa iwapo nahodha
mwenyewe alikuwa ameshikilia
sukani.

Advertisements