Sudan Kusini:Mauaji ya kikabila Bentiu


image

Waasi nchini Sudan Kusini
Umoja wa Mataifa unasema kuwa
vikosi vinavyoipinga serikali nchini
Sudan Kusini viliwaua mamia ya
watu kwa sababu ya kabila lao
wakati vilipouteka mji wa Bentiu wiki
jana.
Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo,
watu hao walilengwa wakiwa katika
maeneo salama walikokuwa
wanahifadhiwa kama vile msikitini,
makanisani na hospitalini.
Umoja huo umesema kuwa
watangazji katika baadhi ya vituo vya
redio walitumia lugha ya chuki na
uchochezi na kuwataka watu wa
kabila fulani kuondoka mjini humo
huku wakiwashauri wanaume
kuwabaka wanawake.
Watu wa kabila laNuer, ni wafuasi
wakubwa wa kiongozi wa waasi na
makamu wa zamani wa Rais Riek
Machar
Wapiganaji wanaomuunga mkono
makamu wa rais wa zamani Riek
Machar waliuteka mji wa Bentiu
ambao ni mji mkuu wa jimbo la Unity
siku sita zilizopita.
Walinda amani wa Umoja wa
Mataifa walilaani kile walichokitaja
kama mauaji yanayowalenga raia
kwa misingi ya ukabila.
Rais Salva Kiir anatoka kabila la
Dinka ambalo ndilo kabila kubwa
kuliko yote nchini Sudan Kusini
Umoja wa Mataifa umesema kuwa
watu ambao hawakuwa wa kabila la
Nuer,waliuawa Bentiu.
credit: BBC

Advertisements