JAY Z NA BEYONCE KUWALIPIA ‘KIMYE’ HONEYMOON YA KWENYE BOTI


image

Waarabu wa pemba huwa na desturi
ya kujuana kwa vilemba, licha ya
maneno maneno kuzagaa huku na
kule tangu Jay Z na Beyonce
kutangaza kutohudhuria harusi ya
Rapa Kanye na kim kwa kile
kilichotajwa kuwa ni kutotaka kuuza
sura kwenye kipindi cha familia ya
Kardashian ‘Keeping up with the
Kardashian’…
Hatimaye wakali hao wa Drunk in
Love, wamefunguka na kukana
shutuma hizo huku wakiahidi
kuwalipia boti ya kifahari aina ya
Yatch, watakayotumia kipindi cha
fungate lao ‘HoneyMoon’, huku kiasi
cha kukodi boti iyo kikitajwa kuwa ni
dola za kimarekani 168,000 bila
chenji.
Mbali na mbwembwe hizo, mmiliki
huyo wa mavazi ya Rocawear
ameahidi kumuangushia bonge moja
ya pati la kibachela(bachelor party)
kwenye moja klabu zake anazomiliki
za 40/40 iliyopo jijini Manhattan
ikiwa ni katika kumuaga rafiki yake
huyo wa kitambo kirefu na
kumkaribisha kwenye maisha ya
mapya.