MTANGAZAJI KANDANDA MKONGWE WA ZAMBIA ‘DENNIS LIWEWE’ AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 78


image

Dennis Liwewe enzi za ujana wake
akitangaza mpira
Mtangazaji mkongwe wa Kandanda
nchini Zambia, Dennis Liwewe
amefariki dunia leo asubuhi katika
hospitali kuu ya Levy mwanawasa
mjini Lusaka zambia.

image

Mtangazaji wa kandanda ‘Dennis
Liwewe’ kipindi cha hivi karibuni
kabla ya kuaga Dunia
Mtangazaji huyo amefariki akiwa na
umri wa miaka 78 baada ya
kusumbuliwa na maradhi ya Ini.
Msemaji wa familia alisema taarifa
zaidi zitatolewa baada ya kikao
kilichofanyika leo mchana.
Liwewe atakumbukwa kwa umahiri
wake wa kutangaza mpira katika
kipindi cha miaka 45 akiwa tayari
ameshatangaza zaidi ya fainali 14 za
kombe la mataifa ya afrika.
Mungu ailaze roho ya marehemu
mahala pema peponi Ameen

Advertisements