Yaliyomo China na Marekani zalaani vita Sudan kusini .


image

Jeshi lilipoteza mji wa Bentiu ambao
sasa uko chini ya waasi
China na Marekani zimelaani ghasia
zinazoendelea nchini Sudan, kufuatia
shutuma kwamba wapiganaji waasi
waliwauwa mamia ya raia katika mji
wenye utajiri wa mafuta wa Bentiu.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa
China amezitaka pande zote husika
kwenye mzozo huo kufanya
mazungumzo ya kisiasa na kuwataka
maafisa wa Sudan Kusini kulinda
maslahi ya Uchina .
Uchina ni muwekezaji mkuu katika
sekta ya mafuta Sudan kusini .
Ikulu ya White house imeelezea
ghasia nchini Sudan kama
zisizokubalika na kwamba zinakiuka
imani ya raia wa Sudan Kusini
waliyokua nayo kwa viongozi wao .
Kadhalika Marekani imesema kuwa
imeshangazwa na mauaji ya
kinyama ya mamia ya raia Sudan
Kusini na kutoa wito wa kusitishwa
kwa msururu wa vurugu
zinazoendelea nchini humo.
Umoja wa mataifa ulisema siku ya
Jumatatu kwamba waasi waliwauwa
mamia ya raia katika mji wa Bentiu
na wengi walikufa katika msikiti
mmoja, hosipitali na kanisa ambako
walikuwa wamekimbilia kutafuta
usalama.
Msemaji wa ikulu ya White House,
Jay Carney, amesema kuwa rais,
Salva Kiir, na kiongozi wa waasi ni
sharti watangaze hadharani kuwa
mashambulizi dhidi ya raia
hayakubaliki.
Maelfu ya watu wamefariki dunia
tangu mapigano ya kikabila yazuke
mwezi Disemba mwaka uliopita.

image

Advertisements