Taarifa kuhusu kocha mpya wa Taifa Stars na lini anakuja Bongo


image

Kocha Mkuu mpya wa Taifa Stars,
Martinus Ignatius Maria maarufu
kama Mart Nooij anatarajiwa
kuwasili nchini Jumamosi alfajiri
(Aprili 26 mwaka huu) tayari kwa ajili
ya kuanza kazi ya kuinoa timu hiyo.
Nooij (59) atawasili saa 7.20 usiku
kwa ndege ya Ethiopia Airlines
ambapo anatarajia kukutana na
waandishi wa habari Jumamosi
mchana, saa chache kabla ya kuanza
mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars
na Burundi itakayochezwa kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
source: TZA