China kutengeneza ‘lifti’ yenye kasi zaidi duniani inayoweza kupanda ghorofa 95 kwa sekunde 45


Kampuni ya Hitachi imetangaza
mpango wake wa kutengeneza lifti
yenye kasi zaidi duniani (The world’s
fastest ultra-high-speed elevator)
katika jengo refu la Guangzhou CTF
Finance Centre linalojengwa huko
Guangzhou, China.

image

Mchoro wa jengo hilo refu la
Guangzhou CTF
Jengo hilo linalotazamiwa
kukamilika ifikapo mwaka 2016,
litakuwa na lift hizo zenye uwezo wa
kwenda kasi ya kupanda au kushuka
ghorofa 95 kwa sekunde 45.
Hitachi wamesema lifti hizo
zitatumia teknolojia ambayo
inahakikisha usalama kwa watumiaji,
hivyo wasafiri watakuwa wakisafiri
salama na kwa raha pamoja na
mwendo wake mkali.

image

Ujenzi wa kikwangua anga hicho cha
CTF ulianza mwaka 2010 na picha
hii ilipigwa 23 December 2012, na
linatarajiwa kukamilika mwaka 2016.
Source: Daily Mail & BONGO5