Davido kutua Dar mwezi ujao kwenye show ya Road to MAMA


Mashabiki wa Davido watakuwa na
wasaa mwingine wa kumshuhudia
staa huyo mwezi ujao kwakuwa
imefahamika kuwa atakuwa
miongoni mwa wasanii watakaokuja
Dar es Salaam kwenye show ya Road
to MAMA.

image

Road to MAMA ni show za utangulizi
za tuzo za MTV Africa ambapo
mwaka huu zitafanyika katika nchi
tatu, Tanzania, Afrika Kusini na
Nigeria.
“Exclusive Kwa wale wapenzi wa
msanii @Davido wakae Tayari kwani
anakuja Tanzania mwezi ujao ktk
sherehe ya Road To MaMa party,”
imesomeka tweet ya kituo kipya cha
redio jijini Dar es Salaam, 93.7 FM

Advertisements